Mr P: Kuvunjika kwa P-Square sababu ni mashabiki

LAGOS: MSANII wa Nigeria Peter Okoye, maarufu kwa jina la Mr P, ameweka wazi sintofahamu zao na pacha wake Paul Okoye aka Rudeboy, akitupia lawama mashabiki wao kuwa ndiyo chanzo cha kuvunjika kwa kundi hilo.
Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha AY Live Show, Mr P amesema ugomvi wao wa muda mrefu kwa wasanii hao waliokuwa wakitamba mno kwa mafanikio ya muziki wao na nje ya muziki wao barani Afrika chanzo kikubwa ni mashabiki kuwalinganisha na kuwashindanisha.
“Mashabiki ndio sababu ya P-Square kutokuwa pamoja tena,” amesema. “Ndugu wawili wakifanya jambo wanafanya jambo moja, halafu watu wanaanza kusema mmoja ni bora kuliko mwingine, mmoja anajawa sifa heshima inakosekana lazima mnatengana.”
Utengano huo, ambao ulianza rasmi mwaka wa 2017, ulikuwa ukiendelea kwa muda mrefu huku kukiwa na tofauti za ubunifu, mizozo kuhusu fedha na usimamizi. Mambo yaliongezeka zaidi kwa kukamatwa kwa Paul kwa kutatanisha na Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC)-tukio ambalo Paulo alidai baadaye lilipangwa na kaka yake mwenyewe, Peter.
Katika mahojiano ya awali, Paul Okoye hakudai tu kuhusika kwa Peter katika kukamatwa kwake lakini pia alisisitiza kwamba alikuwa na jukumu la kuandika nyimbo nyingi za wawili hao. Mr P, hata hivyo, alikataa hadharani dai hilo, akimtaja kaka yake kuwa muongo na kukanusha mabaya yote anayotuhumiwa kuyafanya kwa ndugu yake pamoja na kutokuwa na mchango mkubwa katika kundi lao.
Kuongeza mafuta kwenye moto huo, Paul pia alimshutumu Peter kwa kumvuta kaka yao mkubwa na meneja wa zamani, Jude Okoye, kwenye matatizo ya kisheria. Wakati wa kusikilizwa kwa dhamana ya Jude mnamo Februari, Paul aliwaambia waandishi wa habari:
Hata hivyo mashabiki wanaotuhumiwa kuwa chanzo cha ndugu hao kutengana nao wamerusha dongo kwa ndugu hao kwamba umaarufu waliokuwa nao ulizaa, ubinafsi ndiyo chanzo cha kutengana kwao.




