Mastaa

Mr. P Afichua hofu yake kubwa maishani

LAGOS: MSANII mashuhuri wa R&B kutoka Nigeria, Peter Okoye ‘Mr. P’—amefunguka kuhusu jambo ambalo linamtisha zaidi maishani, akisema kuwa si kifo kinachomtia hofu bali ni umaskini.

Mr. P amesema kuwa hofu hiyo imejengwa na maisha magumu aliyowahi kupitia katika utoto wake, ikiwa ni pamoja na tukio walilowahi kukumbana nalo la kubomolewa nyumba waliyokuwa wakiishi.

“Siogopi kifo. Kitu pekee ninachokiogopa katika maisha haya ni umaskini na kufeli,” amesema msanii huyo ambaye aliunda kundi maarufu la P-Square pamoja na ndugu yake Paul Okoye.

Akikumbuka jinsi familia yao ilivyoishi kwenye chumba kimoja walichokuwa wamekodisha, kabla ya nyumba hiyo kubomolewa ghafla baada ya mwenye mali kuuza kiwanja.

Tukio hilo, ambalo lilitokea wakiwa ndani, limempa kumbukumbu ya maisha ya hali ngumu na ndilo linalomfanya awe mwangalifu na kuogopa kurudi katika umasikini.

Related Articles

Back to top button