Mlinzi wa Yanga atua Geita Gold

DAR ES SALAAM: MLINZI wa zamani wa Yanga Ali Ali ametua Geita Gold FC inayoshiriki Championship.
Geita Gold imemtambulisha mchezaji huyo leo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kikosi chake kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya Championship.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, Ali anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kusaidia timu kufikisha malengo waliyojiwekea ikiwemo kuhakikisha wanapambana ikiwezekana kupanda Ligi Kuu.
“Ali Ali atasaidia kuongeza nguvu ya ulinzi wa Geita Gold, Wapinzani jiandaeni… safari ya kufika golini sasa imeongezewa ulinzi,”ilisema taarifa hiyo.
Ali amewahi kutumikia klabu mbalimbali kama vile Yanga, KMC, Stand United, KVZ na nyingine hivyo, ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa.
Huo ni usajili wa pili kwa timu hiyo baada ya jana kumtambulisha Kocha Mkuu wao mpya ni Zuberi Katwila.