Mitindo

Miss Universe Asia ang’ang’ania taji

FILIPINO: MSHINDI wa Miss Universe Filipino 2025 na Miss Universe Asia, Ahtisa Manalo ambaye ameshiriki mashindano ya dunia ya Miss Universe na kushika nafasi ya tatu ametangaza kwa umma kuwa hana nia ya kuachana na taji la Miss Universe Asia, kamamalivyoshinikizwa hapo awali.

Ahtisa, mwenye umri wa miaka 28, alichagua kuendelea kushikilia majukumu yake kama mshindi wa tatu wa Miss Universe 2025 badala ya kuchukua taji la bara la Asia.

Akizungumza na mashabiki waliokuwa na matumaini makubwa kwake aliwataka wakubali matokeo ya shindano hilo la dunia kwa kueleza kuwa wakubali nafasi ya tatu aliyoshinda licha ya matarajio ya wengi kwamba angeshinda nafasi ya kwanza.

Mashindano ya Miss Universe mwaka huu yalimalizika Npvemba 21 huko Bangkok, Thailand, ambapo Fatima Bosch kutoka Mexico alinyakua taji la ushindi huku warembo kutoka nchini, Thailand, Venezuela, na Ivory Coast wakishika nafasi za pili, nne, na tano kwa utaratibu.

Matokeo hayo yamekumbwa na mjadala mkali miongoni mwa umma, huku baadhi ya watu wakijiuliza kama Bosch alistahili taji hilo ama la! Huku, washiriki kutoka Estonia na Ivory Coast wakidai kutokubaliana na nafasi walizotangazwa kushinda na wakasusia mataji yao.

Kuhusu historia ya Ahtisa, imeripotiwa kuwa mama yake ni Mfilipino-Malenga, na baba yake wa kambo anaasili ya nchi mbili Swedeni na Finlandi.

Ahtisa alikuwa amewakilisha Philippines mwaka 2018 kwenye mashindano ya Miss International, ambapo alishika nafasi ya kwanza miongoni mwa washiriki wote.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button