Mitindo

Miss India amshitaki mumewe adai fidia

MUMBAI: KATIKA tukio jingine, aliyekuwa muigizaji na Miss India, Celina Jaitly, amefungua kesi ya unyanyasaji wa kinyumbani dhidi ya mumewe, Peter Haag, raia wa Austria.

Kesi hiyo iliwasilishwa katika Mahakama ya Andheri, Mumbai, chini ya Sheria ya Ukatili wa Kinyumbani.
Kwa mujibu wa taarifa, Celina anadai fidia ya randi50 crore pamoja na malipo mengine kufidia hasara za kipato na mali alizopoteza.

Celina na Peter wamebarikiwa kuwa na watoto watatu seti mbili za mapacha. Walipata mapacha wao wa kwanza, Winston na Viraaj, mwaka 2012. Mnamo 2017 walipata mapacha wengine, Arthur na Shamsher, ingawa Shamsher alifariki kutokana na matatizo ya moyo.

Celina pia amekuwa akigonga vichwa vya habari kutokana na kukamatwa kwa kaka yake, Meja (mstaafu) Vikrant Jaitly, aliyedaiwa kuzuiliwa kwa njia isiyo halali nchini UAE mwaka 2024.

Wizara ya Mambo ya Nje ya India imethibitisha kuwa inatoa msaada wa kibalozi na kwamba wamemtembelea mara nne.

Mahakama Kuu ya Delhi pia imetoa maagizo kwa serikali kumsaidia Meja Vikrant kwa huduma za kisheria na matibabu, baada ya Celina kufungua ombi rasmi kuomba msaada huo.

Related Articles

Back to top button