EPL

Milner kusepa Liverpool

TAKRIBANI miaka minane sasa mchezaji James Milner anaitumikia Liverpool, na sasa rasmi ataondoka klabuni hapo kujiunga na Brighton Hove Albion.

Taarifa ya mwanahabari, Fabrizio Romano imeeleza kuwa Milner ambaye kwa sasa anacheza beki wa kulia amekubali kujiunga ‘Amex’ kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Sambamba na usijali wa Milner, Brighton pia imenasa saini ya Joao Pedro kutoka Watford kwa uhamisho wa pauni milioni 30.

Uhamisho wa Milner utafuatia na baadhi ya wachezaji, akiwemo Naby Keita, Alex Chamberlain watakaoondoka bure Liverpool baada ya mikataba yao kuisha msimu huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button