Kwingineko

“Messi ni mbaya zaidi akiwa na hasira” – Mascherano

MIAMI, Kocha wa Inter Miami, Javier Mascherano anaamini kwamba nahodha wake Lionel Messi anaweza kubadilisha hasira zake kuwa kiwango bora dhidi ya klabu yake ya zamani ya Paris St Germain katika mechi ya Jumapili ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la Klabu, akimaanisha Muargentina huyo hufanya vizuri zaidi akiwa na jambo la kuthibitisha.

Messi, ambaye alijiunga na PSG mwaka wa 2021 baada ya kuondoka Barcelona na kukaa kwa misimu miwili, alishinda mataji mawili ya Ligue 1 lakini akashindwa kupata taji la UEFA Champions League. Maisha yake katika klabu hiyo yalidhihirishwa na uhusiano mbaya kati yake na mashabiki wa PSG, na Messi baadaye alikiri kuwa “hakuwa na furaha” klabuni hapo.

Mascherano ameiambia ESPN kuwa ni faida kwao mshambuliaji huyo awe na hasira kali anapocheza na PSG akisema pia Messi ni aina ya mchezaji ambaye anafanya vizuri kama kuna kitu kimekwama akilini mwake

“Kwetu sisi, ni bora kama Messi acheze akiwa na hasira. Unajua Yeye ni mmoja wa wachezaji ambao, wakati kuna kitu kimekwama katika akili yake, hutoa kitu cha ziada kidogo.” amesema

Mascherano alikuwa sehemu ya ‘comeback’ maarufu ya Barcelona ya 6-1 dhidi ya PSG katika hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League mwaka 2017 wakati Wakatalonia hao walikuwa wamepoteza mechi ya mkondo wa kwanza kwa mabao 4-0 mjini Paris ikiwa chini ya kocha kocha wa sasa wa PSG Luis Enrique.

Wachezaji kadhaa wa Inter Miami walikuwa sehemu ya pambano hilo kubwa. Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets wote walianza huku Jordi Alba akiwa benchi. Mascherano sasa atakutana na Enrique akiwa kocha katika mchezo wenye msisimko mkubwa hapo Jumapili.

Related Articles

Back to top button