Messi abadili mawazo hatma yake PSG
MSHAMBULIAJI Lionel Messi anafikiria hatma yake katika klabu ya Paris Saint-Germain na ameripotiwa hataki kusaini kuongeza mkataba katika klabu hiyo ya mji mkuu wa Ufaransa.
Mkataba wa sasa wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na mustakabali wake haujulikani.
PSG ilikuwa na inaamini Messi alikuwa akipanga kuongeza mkataba wake kabla ya michuano ya Kombe la Dunia, lakini ubingwa ilioutwaa Argentina unaonekana kuwa muhimu kwa uamuzi wake.
Barcelona sasa inatajwa kuwa kipaumbele kikuu kumsajili messi.
Hata hivyo, moja ya masharti yanayopaswa kuzingatiwa ili aweze kurejea Barca ni kwa Messi kutoa sehemu kubwa ya mshahara wake ili kuendana na hali ya sasa ya klabu hiyo ya Catalonia na kiwango chao cha mshahara.
Klabu nyingine zenye nia ya kumsajili Messi ni pamoja na Inter Miami ya Marekani, Newell’s Old Boys ya Rosario, Argentina na Al-Hilal ya Saudi Arabia.




