Ligi KuuNyumbani

Mchezo wa Kagera vs Singida bila mashabiki

MCHEZO wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara leo kati ya Kagera Sugar na Singida Big Stars katika uwanja wa Kaitaba, Kagera utachezwa bila mashabiki.

Taarifa ya Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imesema uamuzi huo umetokana na sababu za kiusalama baada ya kuthibitika kuwa uzio wa kutenganisha mashabiki na eneo la kuchezea haujakidhi vigezo vya kikanuni.

TPLB imesema baada ya mchezo huo timu ya Kagera Sugar italazimika kuhamia uwanja wa CCM kirumba, Mwanza kwa michezo yake ya nyumbani hadi Kamati ya Leseni za Klabu itakapoukagua uwanja wa Kaitaba na kujiridhisha kuwa mapungufu yaliyoainishwa yamerekebishwa.

Aidha bodi imesema itahakikisha mashabiki wote walionunua tiketi kwa ajili ya mchezo huo wanapata haki yao.

Related Articles

Back to top button