LEO ndio leo pale kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Mbeya City itakapoikaribisha Mashujaa ya Kigoma katika mechi ya mkondo wa pili mtoano kufuzu Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Juni 19 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma Mashujaa iliibuka mshindi kwa magoli 3-1.
Mashujaa imeahidiwa kupewa shilingi milioni sita kwa kila goli itakalofunga katika mchezo wa leo.
Mshindi wa jumla atafuzu kucheza Ligi Kuu msimu wa 2023/2024.




