Kwingineko

Mbappe kama Ronaldo tu – Ancelotti

MADRID: Meneja wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Real Madrid, Carlo Ancelotti amemwagia sifa mshambuliaji wake Kylian Mbappe akisema kuwa mshambuliaji huyo ana sifa kama za nyota wa Al Nassr FC ya Saudi Arabia Cristiano Ronaldo.

Ancelotti amesema Mbappe anao uwezo wa kumfikia Ronaldo ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa mabingwa hao mara 15 wa UCL akiwa na magoli 451 katika michezo 438.

“Ana nafasi ya kuzifikia namba zake (Cristiano Ronaldo) lakini ana kazi ya kufanya kufika huko kwa sababu Ronaldo ameweka standards zake juu sana lakini (Mbappe) anafuraha kucheza hapa najua anaweza kumfikia Ronaldo” amesema Ancelotti

Akizungumzia kiwango chake ushambuliaji Kylian Mbappe aliyefunga mabao 256 katika michezo 308 aliyocheza PSG, amesema hakujali chochote kuhusu kuwa mshambuliaji bora wa Champions League kama haikuwa njia ya yeye kutwaa makombe.

“Nilikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu uliopita, lakini nilishinda taji? Hapana. Sijali kuhusu kuongoza orodha ya wafungaji, katika ‘Career’ yangu nimefunga mabao mengi sana lakini nitaweka alama iwapo kama magoli haya yatazaa makombe, naweza kufunga hata mabao 50 lakini ninataka kushinda makombe”amesema Mbappe

Mbappe alifunga hattrick ambayo iliihakikishia Real Madrid siti kwenye hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League nyumbani Santiago Bernabeu mbele ya mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester city Real ikishinda kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-3

Related Articles

Back to top button