Featured

Mbappe hana furaha PSG

NYOTA wa soka Kylian Mbappe kwa hisia anataka kuondoka Paris Saint-Germain Januari, 2023 kwa sababu uhusiano wake na klabu hiyo ya Paris umeharibika lakini hataruhussiwa kujiunga na Real Madrid.

Gazeti la michezo, Marca la Hispania limeripoti kuwa Mbappe ameiambia PSG anataka kuondoka Julai 2023 huku Real Madrid iliyowasilisha ombi la pauni milioni 154 sawa na shilingi bilioni 395.3 wakati wa majira ya joto kabla ya kukataa kusajiliwa miamba hiyo ya Hispania ikionesha nia.

Kwa mujibu wa Marca PSG imekubali kufanyia kazi mpango wa Mbappe kuondoka iwapo masharti kadhaa yatatimizwa ikiwemo kwamba uhamisho kwenda Bernabeu ufutwe kwenye meza ya mazungumzo.

Katika miaka ya hivi karibuni Mbappe amekuwa akihusishwa kujiunga na Liverpool huku Mfaransa huyo akiripotiwa kuwa na nia ya kujipima Ligi Kuu Uingereza.

Nyota huyo wa kifaranza mwenye umri wa miaka 23 alisaini mkataba na PSG wenye thamani ya pauni 650,000 sawa na shilingi bilioni 1.6 kwa wiki majira ya joto lakini mkataba huo haujazuia uvumi kuhusu hatma yake.

Related Articles

Back to top button