Kwingineko

Max, Abuya, kunogesha tamasha la Mwamnyeto, Mauya

DODOMA: TAMASHA la michezo lililoandaliwa na wachezaji wawili Bakari Mwamnyeto na Zawadi Mauya linatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ya Julai 13 mkoani Dodoma.

Zawadi Mauya amesema licha ya kupungua kwa wadhamini, maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na litafanyika kwa ubora unaohitajika.

Mauya aliwataka mashabiki wa soka mkoani Dodoma na mikoa jirani kufika katika mchezo huo utakaowakutanisha timu Mauya na timu Mwamnyeto kwa kuwa fedha zitakazopatikana zitaelekezwa kusaidia wenye uhitaji wa akili katika hospitali ya Mirembe iliyopo mkoani humo.

“Taasisis yetu ni kwa ajili ya kuasiaidia wenye uhitaji haiiingizi faida hivyo furaha na lengo letu ni kuwakutanisha mashabiki pamoja na kuchangia wenzetu kadri tutakavyoweza, tunawaomba wapenda soka waje kwa wingi ili lengo la kuwasaidia wenye uhitaji wa akili pale hospitali ya Mirembe ifanikiwe,” alisema Mauya.

Katika mchezo huo wachezaji mbalimbali wanaocheza timu kubwa wakiwemo Mukoko Tonombe kutoka Congo, Obrey Chirwa, Max Nzengeli, Duke Abuya na wengine wengi watakuwepo kunogesaha tamasha hilo.

Tamasha hilo la Bakari Mwannyeto na Zawadi Mauya ni tamasha la tatu kufanyika ambalo tamasha la msimu wa kwanza lilifanyika mkoani Tanga, tamasha la pili lilifanyika mkoani Mbeya na tamasha la msimu wa tatu linatarajiwa kufanyika mkoani Dodoma.

Related Articles

Back to top button