Ligi KuuNyumbani

Mashabiki Yanga kutoa heshima dakika ya 43

MASHABIKI wa klabu ya Yanga leo watasimama na kupiga makofi dakika 43 katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC kutoa heshima kwa benchi la ufundi la klabu hiyo kutopoteza michezo 43.

Benchi la Ufundi la Yanga linaongozwa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabiakisaidiwa na Cedric Kaze.

“Ikifika dakika ya 43 kwenye mchezo wetu wa leo dhidi ya KMC FC Mashabiki tutasimama na kupiga makofi kutoa heshima kwa Kocha Nabi na benchi lake la Ufundi kwa kucheza michezo 43 bila kupoteza” amesema Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe.

Mara ya mwisho Yanga kupoteza mechi katika ligi hiyo ilikuwa ni Aprili 25, 2021 ilipolala kwa bao 1-0.

Related Articles

Back to top button