EPLKwingineko

Mancity yajitosa vita ya Rice

KLABU ya Manchester City  imewasilisha ofa ya kumtaka kiungo wa West Ham United Declan Rice

Mancity wameripotiwa kuwasilisha dau la Pauni milion 80  pamoja na ongezeko la pauni milioni 10 dili litakapokamilika kitita ambacho kinaweza kuwakosha West Ham United na wakakubali kumpiga bei kiungo huyo wa kimataifa wa England.

Washika mitutu wa London Arsenal walikuwa katika hatua nzuri za kuinasa Saini ya Rice ambapo waliwasilisha ofa ya pauni milioni 75 iliyokataliwa na West Ham na sasa wanasubiriwa kurudi na ofa nyingine nono zaidi.

West Ham United wao waliweka wazi nia yao ya kumuweka sokoni nyota huyo kwa dau la pauni milioni 100 hivyo kinachosubiriwa ni msimamo wao juu ya ofa iliyotumwa na Manchester City lakini pia ofa nyingine itakayowasilishwa na Arsenal.

Related Articles

Back to top button