Tetesi

Man City macho kwa Hakimi

MABINGWA wa Ligi Kuu England, Manchester City imeripotiwa kuwa na nia ya kumsajili beki wa kulia wa Paris Saint-Germain, Achraf Hakimi majira haya ya joto na inaandaa kulipa kiasi kikubwa cha fedha kupata saini yake.

Kwa mujibu wa mtandao wa michezo wa Hispania, Marca, Hakimi mwenye umri wa miaka 24 ametambuliwa kama mbadala sahihi wa Kyle Walker wakati Kocha Pep Guardiola akitaka kuimarisha safu ya ulinzi ya City kulinda mataji matatu klabu hiyo iliyoyatwaa msimu uliopita.

Walker ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake anatarajiwa kujiunga na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich majira haya ya joto.

Achraf Hakimi ameshinda mataji mawili ya Ligue 1 tangu ajiunga na PSG mwaka 2021 akitokea Inter Milan.

Related Articles

Back to top button