Nyumbani

Makombe ya Yanga kwa Mama Karume

UONGOZI wa Yanga chini ya Rais Eng Hersi Said, Benchi la ufundi na wachezaji leo wamemtembelea Mama Fatma Karume pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini na kuwakabidhi makombe manne ilyoshinda msimu uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Yanga hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Mama Karume, maeneo ya Maisara, Zanzibar imekuwa ni mara ya kwanza kwa uongozi wa Yanga kukutana na Bodi ya Wadhamini tangu timu hiyo ilipobeba makombe hayo mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mama Karume amewapongeza wachezaji kwa mafanikio hayo ya kubeba mataji manne ya mashindano ya ndani.

“Nimefurahi sana na ninawapongeza sana wachezaji wetu kwa kupambana kwa nia moja kuhakikisha Yanga inabeba makombe yote haya manne, hii ni heshima kubwa kwa klabu yetu yenye historia kubwa Afrika nzima,” amesema Mama Karume.

Mama Karume amewasihi wachezaji kupambana zaidi kwa ajili ya kufanya vizuri zaidi na kwenye michuano ya kimataifa.

Related Articles

Back to top button