Majibu ya Chalamet yawachanganya mashabiki

CALIFORNIA: MUIGIZAJI Timothee Chalamet ambaye pia ni mwanamuziki akiwa kwenye mahojiano na Samuel Goldwyn Theatre huko Beverly Hills, azidisha uvumi kwamba anaweza kuwa rapper wa Uingereza asiyejulikana EsDeeKid.
Tetesi mbalimbali zinahusu utambulisho wa mwanamuziki huyo maarufu, ambaye amekua akifananishwa na rapa EsDeeKid ameonekana akisuasua na majibu yake akiwa na mtangazaji Samuel alipomuuliza “Mashabiki wako wamepoteza akili na wanasema kuwa wewe ni EsDeeKid,” na Chalamet jibu lake lilikuwa moja tu “no comment”.
Pamoja na kulinganisha macho yao, mashabiki pia wamebainisha kuwa wanavaa nguo zinazofanana, ikiwa ni pamoja na skafu ya alama za fuvu.
Mwaka 2019 Chalamet alifichua kwenye “The Graham Norton Show” kwamba aliwahi kurap alipokuwa shuleni na alitambulika kwa jina la “Lil Timmy Tim.”
Hata hivyo mashabiki wanaeleza kuwa, Chalament akiwa moja kati ya waigizaji walioteuliwa mara mbili na tuzo za Oscar, basi anaweza kuwa na ujuzi mkubwa sana katika tasnia hii ya sanaa.




