Maandalizi duni yametugharimu-Minziro


KOCHA Mkuu wa Geita Gold, Fred Minziro amesema timu yake imetolewa mapema kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kukosa maandalizi mazuri.
Akizungumza na Spotileo, kocha huyo amesema wachezaji wa timu hiyo wamepambana kwa kadri ya uwezo wao lakini ilishindikana hivyo Geita inakwenda kujipanga.
“Imetuuma kutolewa mapema lengo ilikuwa tufike hatua ya makundi na uwezo huo tunao, tumekubali matokeo na tunarudi kwenye ligi kutafuta nafasi nyingine mwakani,” amesema Minziro.
Amesema anafurahi kuona uongozi unatoa sapoti kubwa katika mambo mbalimbali na anaamini mwakani timu itarudi tena kwenye michuano hiyo.
Mbali na kutolewa kwenye mashindano ya kimataifa pia Geita Gold, haijawa na matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu bara ikiwa imecheza mechi nne, kutoka sare mara 3 na kupoteza mmoja.