EPL

Lopetegui Kocha mpya West Ham

KLABU ya West Ham United ‘The Hammers’ imetangaza kumteua Julen Lopetegui kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo.

Lopetegui anachukua mikoba toka kwa David Moyes aliyeondoka West Ham mwisho wa msimu uliopita wa Ligi Kuu England.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania, klabu za Porto, Real Madrid, Sevilla na Wolverhampton Wanderers ataanza kazi rasmi The Hammers Julai Mosi.

Akizungumza na Televisheni ya West Ham Lopetegui ameonesha furaha yake katika kuendeleza misingi imara iliyowekwa na kuongeza vionjo vyake klabuni.

“Najihisi furaha sana, kwanza kabisa, kuweza kuwa sehemu ya hatima ya klabu hii kubwa,” Lopetegui amesema.

Lopetegui ataungana a Kocha Mkuu Msaidizi Pablo Sanz, Kocha Msaidizi na Mkuu wa Utendaji Oscar Caro, Kocha Msaidizi na Mkuu wa Uchambuzi Juan Vicente Peinado, Kocha wa utimamu wa mwili Borja De Alba na Kocha wa Ufundi, Edu Rubio.

Xavi Valero ataendelea na jukumu lake la ukocha wa magolikipa wa kikosi cha kwanza cha timu ya wanaume.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button