EPL
Liverpool yatambulisha uzi mpya

KLABU ya Liverpool imezindua jezi mpya za nyumbani zitakazotumika msimu wa EPL na michuano mingine msimu wa 2023/2024 utakaoanza Agosti, 2023.
Liverpool bado ina mkataba na kampuni ya Nike ambayo ndiyo watengenezaji wa jezi hizo, lakini pia inaendelea kudhaminiwa na mdhamini mkuu Benki ya Standard Chartered.
Upande wa kushoto mwa jezi hiyo bado wanaendelea kuwatangaza Expedia.
Jezi hizo ni chaguo la kwanza, hivyo muda wowote kuanzia sasa watazindua jezi za ugenini na zile za chaguo la tatu.