Ligi Ya WanawakeNyumbani

Ligi Daraja la Kwanza Wanawake yaanza leo

Ligi Daraja la Kwanza Wanawake (WFDL) 2023 inaanza leo kwa mechi sita kupigwa mkoani Mwanza.

Katika kundi A Bunda Queens itaavana na Masala Queens huku Mapinduzi Queens ikimenyana na Lengo Queens kwenye uwanja wa Nyamagana.

Nazo Mlandizi Queens itakuwa uwanjani kukabiliana na JMK Park kwenye uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo wa kundi B.

Uwanja wa CCM Kirumba pia utashuhudia Singida Warriors ikipambana na Ukerewe Queens huku Bilo ikichuana na TSC Queens katika kundi C.

Katika kundi D Geita Gold Queens na Mt Hannang Queens zitatimua vumbi kwenye uwanja wa Nyamagana.

Related Articles

Back to top button