Ligi KuuNyumbani

Lavagne asifu wachezaji Azam

KOCHA Mkuu mpya wa kikosi cha Azam, Denis Lavagne amesema hadhani kama atakuwa na kazi ngumu kwenye kibarua chake kutokana na ubora wa wachezaji wa timu hiyo.

Akizungumza na Spotileo, akiwa kwenye mazoezi ya kwanza ya timu hiyo, kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kwa saa chache alizofanya mazoezi na timu hiyo amegundua timu hiyo ina wachezaji wenye vipaji.

“Nimewaona wachezaji kwenye mchezo dhidi ya Yanga lakini pia nimefanya nao mazoezi kwa mara ya kwanza nimevutiwa na spiriti yao wamenionesha utayari,” amesema Lavagne.

Amesema kitu kikubwa anachotarajia kukifanya ni kupandikiza mifumo yake kidogo kidogo wakati ligi ikiendelea.

Kwa mujibu wa Lavagne falsafa yake ni kutaka timu yake icheze soka la burudani na kufunga mabao mengi na hilo linawezekana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button