Kufuru ya Saudi Arabia yamtibua Neville

NAHODHA wa zamani wa Manchester United Garry Neville ametoa wito kwa watendaji wa Ligi Kuu ya England kupiga marufuku uhamisho kwenda Saudi Arabia ili kuhakikisha uadilifu katika mchezo wa soka.
Neville ametoa kauli hiyo baada ya msururu wa uhamisho wa wachezaji katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati,ambapo majina makubwa kama Karim Benzema na N’golo Kante walikamilisha uhamisho wa kwenda kucheza ligi ya Saudi arabia ‘Saudi Pro League’.
Mwezi Juni, Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF), ambao unamiliki klabu ya Newcastle United ulitangaza kununua timu nne nchini humo ikiwemo Al Nassr anayokipiga Cristiano Ronaldo.
“Ligi Kuu ya England inapaswa kuweka vikwazo kufanyika uhamisho kwenda Saudi Arabia ili kuhakikisha uadilifu wa michezo haupotei,” amesema Neville.
				
					



