Kongamano wapiga picha kufanyika Juni

KONGAMANO maalum la wapiga picha mnato na video kufanyika Juni 6, mwaka huu Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habani Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Big Solution Rajab Mchatta amesema lengo kuu la kongamano hilo ni kuwaleta pamoja na kujadili changamoto zilizopo katika tasnia yao.
Mchatta ameongeza kuwa kongamano hilo litawakutanisha wapiga picha na wakufunzi ambao watatoa elimu ya masuala ya maadili, fursa za biashara na matumizi ya teknolojia.
Moja wa wapiga picha nguli nchini ambaye ni Mdhamini wa kongamano hilo Mkurugenzi wa DTP Hanif Abdulrasul amesema amevutiwa sana na wazo hilo na kusema kuwa litasaidia wapiga picha kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo elimu ya kuwekeza katika bima ya vifaa vya uzalishaji picha.
Naye Haika Lawele, Mkurugenzi wa Mbezi Garden Hotel, ambao ni wadhamini wa ukumbi amesema wametoa eneo hilo kuanzia asubuhi hadi jioni ili kufanikisha tukio hilo la kuwakutanisha wapiga picha na kupata elimu ya maadili ya picha ili kuongeza ubora katika kazi zao.



