Kwingineko

Kocha Atalanta amjia juu Lookman

Amtaja kama mmoja ya wapiga penati wabovu zaidi aliowahi kuwaona

LOMBARDY: KOCHA mkuu wa Atalanta Gian Piero Gasperini amemtolea maneno makali mshambuliaji wake Ademola Lookman baada ya mchezaji huyo aliyeingia kutokea bench kukosa penati iliyosababisha miamba hiyo ya Serie A kuaga kwenye michezo ya ‘playoff’ kwa jumla ya mabao 5-2 mbele ya Club Brugge kwenye Champions League jana usiku.

Lookman aliingia kutoka benchi na kuwapa Atalanta matumaini baada ya kufunga bao sekunde 42 baada ya kuingia lakini baadaye alikosa penati ambayo iliokolewa na golikipa wa Brugge Simon Mignolet.

Baada ya mchezo Gasperini hakutafuna maneno hata kidogo akiuponda uwezo wa mshambuliaji huyo kufunga penati na kusema kuwa hakutumwa kupiga penati hiyo na mtu yeyote.

“Lookman hakustahili kupiga penati ile, ni mmoja wapigaji wa ovyo sana wa penati kuwahi. Kiukweli ana rekodi mbovu sana hata mazoezini anafunga chache sana. Retegui na De Ketelaere walikuwepo lakini Lookman katika nyakati kama zile akaamua kuchukua mpira, kitendo kile sikupenda hata kidogo” amesema Gasperini

Atalanta wanaondoka katika hatua hiyo licha ya kupewa nafasi kubwa ya kuvuka kwenda hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Related Articles

Back to top button