
KLABU ya KMC imevunja benchi la ufundi la timu hiyo baada ya kufikia makubaliano.
Taarifa ya KMC imesema uongozi wa timu hiyo umefikia makubaliano na Kocha Jamhuri Kihwelo Julio ambaye atachukua timu akiwa na benchi lake la ufundi.

“Bodi ya timu ya manispaa ya kinondoni(KMC) baada ya kukaa kikao mapema leo asubuhi imeamua kuvunja benchi lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha THIERY HITIMANA baada ya kufikia makubaliano kutokana na kutoriridhishwa na mwenendo wa wa timu msimu huu,”imesema taarifa hiyo.
KMC inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 26 baada ya michezo 26.