Kwingineko

Kivumbi Real Madrid vs Chelsea ulaya leo

LIGI ya Mabingwa Ulaya inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Hispania na Italia.

Jijini Madrid, Hispania miamba Real Madrid itakuwa mwenyeji wa Chelsea ya England kwenye uwanja Santiago Bernabeu katika mchezo unaotarajiwa kuwa kivutio.

Napoli inayoongoza ligi kuu Italia, Serie A itakuwa mgeni wa AC Milan pia ya Italia kwenye uwanja wa San Siro.

Katika mechi za robo fainali mbili za kwanza Aprili 11, miamba ya soka Ujerumani, Bayern Munich imepokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Manchester City kwenye uwanja wa Etihad.

Nayo Inter ya Italia ikicheza ugegeni imeipa kipigo cha mabao 2-0 Benfica ya Ureno.

Related Articles

Back to top button