Europa

Kisa Medali za Spurs UEFA yaomba radhi

ZURICH: SHIRIKISHO la soka barani ulaya UEFA limeomba radhi kufuatia baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Tottenham Hotspur kukosa medali za washindi wakati wa hafla ya kuwakabidhi kombe kwenye fainali ya Europa League Jumatano baada ya wachezaji wengi kuliko ilivyotarajiwa kuingia kwenye foleni ya wavaa medali.

Nahodha wa Spurs Son Heung-min na wachezaji wengine wawili, waliokuwa wa mwisho kujipanga kuvaa medali, walitoka mikono mitupu baada ya timu yao kuifunga Manchester United 1-0 na kushinda kombe la nne la Europa klabu hiyo Jumatano huku nahodha huyo akinyanyua kombe bila medali shingoni mwake.

“Kwa masikitiko makubwa tunapenda kuwafahamisha wapenzi wa soka kuwa, hatukuwa na medali za kutosha jukwaani wakati wa utoaji wa kombe kutokana ongezeko lisilotarajiwa katika idadi ya wachezaji. Wachezaji zaidi wakiwemo wachezaji majeruhi walishiriki katika sherehe hizo za kukabidhi kombe kuliko ilivyotarajiwa hapo awali” imesema taarifa ya UEFA iliyonukuliwa na BBC

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Medali zilizokosekana ikiwemo ile ya Nahodha Son zilipelekwa haraka kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Tottenham, huku ikiiomba radhi klabu hiyo kwa uzembe mdogo kwenye usimamizi na maandalizi ya Sherehe.

Related Articles

Back to top button