Kwingineko

Kifo cha Jota: Bendera nusu mlingoti Anfield

LIVERPOOL: Majogoo wa jiji Liverpool wameshusha bendera za klabu hiyo hadi nusu mlingoti katika viunga vya Anfield kama ishara ya kuomboleza kifo cha Mshambuliaji wao Diogo Jota aliyefariki katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo karibu na mji wa Zamora nchini Hispania.

Picha na video kutoka katika vyombo vikubwa vya Habari nchini England zimeonesha watumishi wa Anfield, uwanja wa nyumbani wa Liverpool wakishusha bendera hizo hadi nusu mlingoti licha ya taarifa rasmi ya klabu hiyo kutotaja hatua hiyo.

Klabu ya soka ya Liverpool katika taarifa yake imesema imesikitishwa sana na kifo cha Diogo Jota aliyefariki katika ajali ya gari karibu na Zamora kaskazini magharibi mwa Hispania na kuahidi kuheshimu faragha yake kwa kutosema chochote mpaka familia itakapokuwa tayari.

Katika hatua nyingine kamati ya mashindano ya Euro 2025 kwa Wanawake yanayoendelea nchini Switzerland imesema mechi zake za leo usiku zitakuwa na dakika moja ya ukimya kuomboleza kifo cha Jota ambacho ni pigo kubwa kwenye Ulimwengu wa soka

Related Articles

Back to top button