EPL

Kichwa cha Nuno ni Champions league tu

LONDON:MENEJAwa Nottingham Forest Nuno Espirito Santo amesema kikosi chake kilikuwa kikiiwaza nafasi ya kucheza Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya wakati kikosi chake kilipoiduwaza Tottenham Hotspur mabao 2-1 nyumbani kwao katika mchezo wa ligi kuu jana usiku.

Akizungumza baada ya mchezo huo Nuno amesema kikosi chake kimejipata katika mapambano ya nafasi 5 za juu ambazo moja kwa moja msimu ujao zitahusika na Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya taifa la England kuongezewa pointi zinazoiwezesha ligi kuu nchini humo kupeleka timu tano na anasema hawana budi kuipambania.

“Tupo kwenye vita ambayo hakuna aliyeitarajia, tupo Katikati ya timu kubwa na hilo pekee ni la kujivunia, tunaichukua changamoto hii na tutapambana kuishinda. Tulicheza dhidi ya Spurs tukiwa na wazo hili kichwani” Espirito Santo amesema

Nottingham Forest walichukua uongozi wa mapema wa mchezo huo baada ya kupata goli mbili ndani ya dakika 16 za mwanzo kutoka kwa Elliot Anderson na Chris Wood kabla ya Tottenham kuukamata mchezo huo na kuumiliki kwa kiwango kikubwa huku wakipiga mashuti 22 yaliyozaa bao 1 tu la Richarlison kwa manne ya Forest mawili yakizama kambani.

Forest wamerejea nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa kwenye mbio za kuwania nafasi ya Ligi ya Mabingwa huku wakiwa na nafasi ya kuondoka na Kombe msimu huu watakapojibu maswali ya Manchester City katika mchezo wa nusu fainali ya FA Cup wikiendi hii.

Related Articles

Back to top button