Habari Mpya

Kibu kajificha huku!

DAR ES SALAAM: IKIWA Sintofahamu juu ya mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis kutokuwepo kambini nchini Misri inaendelea, Meneja na Msimamizi wa nyota huyo, Carlos Mastermind amesema Kibu Denis na haidai kitu chochote klabu ya Simba na kuwa yupo Ulaya.

Kibu aliyeongeza mkataba wa miaka miwili msimbazi, bado hajajiunga na timu hiyo iliyopo nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao hali ambayo imeleta maswali mengi lakini wenye Simba yao wameamua kuliweka wazi.

Meneja wa mchezji huyo amesema anachofahamu ni kuwa nyota huyo alikuwa Tanzania kukabiliana na changamoto za hati yake ya kusafiria na baadae ameenda Ulaya.

Amesema Kibu alienda Ulaya kwa ajili ya mapumziko na familia yake, akarejea nchini na kufatilia hati ya kusafiria ilikuwa na changamoto baadae akapata matatizo ya kifamilia na kwenda Kigoma.

“Ni kweli kibu hajajiunga na timu Misri kwa sasa yupo Ulaya, ninachojua kuwa hawadai Simba wamemalizana na suala la kwanini hajajiunga na wenzake nchini Misri, Simba wanauwezo wa kulijibu hilo,” amesema Carlos.

Naye Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally umeweka wazi kwamba hati ya kusafiria ndiyo kikwazo cha mshambuliaji wao Kibu Denis kutokujiunga kambini na timu hiyo iliyo nchini Misri.

Amesema nyota huyo hana shida na uongozi bali amekutana na changamoto zake binafsi ikiwamo hati yake ya kusafiria kujaa na anatarajiwa kuungana na wenzake kambini mapema wiki hii kwa ajili ya kuendelea na maandalizi wakati huu wakijiandaa na Tamasha lao la Simba Day.

Amesema Mchezaji huyo haidai Simba kitu chochote kama baadhi ya wadau wa Soka wanavyodhani na badala yake tatizo kubwa ni hati yake ya kusafiria jambo ambalo wanaendelea kulishughulikia kwa ukaribu zaidi.

“Kibu haidai Simba chochote kama wengine wanavyodhani, ila hati yake ya kusafiria imejaa anafanya mchakato, aliomba ruhusa ya kuchelewa kujiunga kambini kutokana na changamoto hiyo na tukamuelewa ila tunatarajia kumuona muda wowote,” amesema Ahmed.

Related Articles

Back to top button