Muziki

Khaligraph Jones kuja na albamu ya kukera

NAIROBI, Kenya: MWANA Hip Hop bora katika Tuzo za Afrimma 2020, Brian Omollo maarufu Khaligraph Jones ametangaza kuja na albamu mpya huku akitoa tahadhali kwa wanaomchukia akiwataka kutojihusisha na albamu hiyo kwa kuwa haitowafurahisha kuanzia wimbo wa kwanza hadi wa mwisho.

Rapa huyo aliyetamba na wimbo wa ‘Mazishi’ na ‘Yego’ alitoa albamu yake ya kwanza Juni 2018.

“Albamu yangu ijayo itasababisha migogoro kuanzia wimbo wa kwanza hadi wa mwisho. Watu wasionipenda waepuke kuisikiliza albamu hiyo sababu haitowafurahisha kutokana na vitu vya kweli nilivyoviandika humo.

“Sijashiriki kikamilifu katika muziki kwa muda mrefu, kutokana na sababu mbalimbali lakini mambo kadhaa yalipaswa kufanywa na yamefanywa hivi karibuni kila kitu kitakuwa wazi na tutaheshimiana kupitia albamu hiyo,” alisema Kaligraph.

Umahiri wa kuimba wa Khaligraph umempa mataji kama vile rapa bora nchini Kenya na Nigeria.

Kaligraph anatumia lugha ya kiingereza na Kiswahili katika tungo zake huku akiamini kwamba lugha ya kiingereza imemsaidia zaidia kupata shoo nyingi za nje ya Kenya.

“Sitadanganya. Nilianza kugundua kurap kwa Kiingereza kunanisaidia baada ya kuanza kusafiri nje ya Kenya na kuona jinsi baadhi ya nyimbo zangu zilivyokuwa zikipendwa nje ya Kenya. Nilifanya vizuri sana nyumbani na nilipokelewa vyema nje ya nchi,” alisema

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button