EPL

Kerkez asaini mitano Anfield

LIVERPOOL, Mabingwa wa Ligi kuu ya England Liverpool FC wametangaza kumsajili beki wa kushoto wa Hungary Milos Kerkez kutoka Bournemouth.

Klabu hiyo bingwa ya soka la England imekubali kulipa ada ya pauni milioni 40 ili kunasa saini ya beki huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa mkataba wa miaka mitano, ikiwa ni usajili wao wa tatu katika kipindi hiki cha usajili baada ya kiungo Florian Wirtz na beki wa pembeni Jeremie Frimpong kutoka Bayer Leverkusen.

Taarifa iliyotolewa na Liverpool imemnukuu Kerkez akisema kuwa ni heshima kwake kucheza ndani ya klabu hiyo ya Merseyside huku akishindwa kuficha furaha yake ya kutua ndani ya klabu hiyo yenye vinasaba na makombe.

“Ni heshima kubwa sana kwangu kucheza katika klabu hii kubwa si tu England bali Duniani, kwakweli nina furaha kubwa sana. Nitaenda nyumbani kwetu katika mji niliozaliwa kupumzika kwa siku chache, kisha nitarudi hapa kuvaa vifaa vya mazoezi na kuanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.” amesema

Kerkez amejiunga na Liverpool baada ya misimu miwili ya kuvutia akiwa Bournemouth ambapo alicheza mechi 74. Mzaliwa huyo wa Serbia ameichezea Hungary mara 23 tangu alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Ujerumani mwaka 2022.

Related Articles

Back to top button