Featured
Kaze Mkurugenzi U17-20, Yanga Princess

KLABU ya Yanga imemteua Kocha Msaidizi wa timu hiyo Cedric Kaze kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu za vijana na Yanga Princess.
Yanga imetoa taarifa hiyo leo kupitia mitandao yake ya kijamii.
“Uongozi wa Yanga SC umemteua Kocha Msaidizi Cedric Kaze kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu za vijana chini ya miaka 17-20 na Yanga Princess huku akiwa anaendelea na majukumu yake kama Kocha Msaidizi kwenye timu kubwa,” imesema taarifa hiyo.
Yanga imesema lengo kubwa la uongozi wa Yanga kumpa Kaze jukumu hilo ni kutaka kuwa na falsafa moja kuanzia soka la vijana, wanawake hadi timu kubwa.