Ligi KuuNyumbani

Kaze: Kesho ni sikukuu

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amewaita mashabiki wa timu hiyo kwenye mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Kocha Kaze anasema Juni 9 ni sikukuu kwa Wananchi, Yanga.

“Tumekuwa na safari nyingi na mechi zenye huzuni na furaha kwetu…kesho ni mchezo wa mwisho wa ligi  na ni sikukuu na siku ambayo tunakwenda kusheherekea mafanikio yetu msimu huu,” amesema kaze.

Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda.

Kwa upande wa wekundu wa msimbazi Simba salamu za kuaga msimu zimetumwa na Kocha Msaidizi, Juma Mgunda ambaye anawatahadharisha wapinzani wao Coastal Union.

“Tunajua itakuwa mechi ngumu, Coastal ni timu nzuri na inahitaji ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri, nasi malengo yetu ni kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Mgunda.

Mechi za kufunga pazia la ligi kuu zitapigwa kwa wakati mmoja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button