Kamwe aitisha Real Bamako
AFISA Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe amesema wapinzani wao Real Bamako watakwenda kusimamulia kwao kitakachowakuta katika mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho Afrika kundi D utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Machi 8.
Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1.
“Tunataka Real Bamako wakiondoka Tanzania waende wakawaambie watu wa nchi yao kwamba wamekutana na Klabu yenye mashabiki bora Afrika,”amesema Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe.
Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 4 baada ya michezo mitatu huku vinara wa kundi US Monastir ikiwa na pointi 7, TP Mazembe nafasi ya tatu pointi 3 na Real Bamako yenye pointi 2.
Kamwe amesema Kauli mbiu ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Real Bamako ni “𝗞wa Mkapa Full Shangwe.”




