Kadansee la Mama ni kesho Leaders Club

DAR ES SALAAM: TAMASHA la Muziki wa Dansi maarufu kama Kadansee la Mama Samia linatarajia kufanyika kwa Kishindo katika viwanja vya Leaders Club, kesho Februari 1, 2025 kuanzia saa 12 jioni.
Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo la Muziki wa Dansi, imekutana na kujadili maandalizi ya mwisho kuelekea tukio kesho linalotarajiwa kuwa la aina yake.
Maandalizi yakiongozwa na Katibu Mtendaji wa BASATA, Dk Kedmon Mapana, kikihusisha pia wajumbe kutoka BASATA, viongozi wa bendi mbalimbali za muziki wa dansi, na wadau wengine wa sanaa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kamati, tamasha hilo linalenga kuonesha utofauti wa muziki wa dansi na kuwaunganisha mashabiki wa burudani kupitia maonesho ya bendi maarufu na wanamuziki mahiri wa Tanzania.
Mashabiki wa muziki wanahimizwa kuhudhuria kwa wingi ili kushuhudia usiku wa burudani ya hali ya juu na kusherehekea sanaa ya muziki wa dansi, inayotambulika kama urithi wa kitamaduni wa taifa.
,,”Jiandae kushuhudia miondoko ya dansi, sauti za kuvutia na burudani ya kiwango cha juu katika Kadansee la Mama Samia,”ilisema taarifa.