Kwingineko

Juventus yaifunza soka Al Ain

WASHINGTON; Vijana wa kocha Igor Tudor Randal Kolo Muani na Francisco Conceicao waliingia kambani mara mbili Juventus ikiichakaza Al Ain ya Kalme za Kiarabu (UAE) mabao 5-0 alfajiri ya leo Alhamisi kwenye mechi yao ya ufunguzi ya Kombe la Dunia la Klabu kwa kundi G Jijini Washington.

Miamba hiyo ya Italia, ambao awali walimtembelea Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya White House, wamepanda hadi kileleni mwa Kundi G juu ya Manchester City, ambao waliwafunga Wydad AC ya Morocco 2-0 katika mchezo wa awali wa kundi hilo.

Wachezaji wa Juventus walikaa kimya muda wote katika ziara yao White House kukwepa Hoja za Trump lakini walikuwa na furaha zaidi kuongea kwa vitendo uwanjani walipoisambaratisha Al Ain kwenye dimba la Audi lililopo jijini Washington.

Kolo Muani, ambaye aliongeza mkopo wake kutoka Paris Saint-Germain ili kucheza michuano hiyo nchini Marekani, alianza kufunga dakika ya 11 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Alberto Costa.

Juventus ya Igor Tudor walipata bao la pili dakika 10 baadaye wakati Conceicao, ambaye pia yupo kwa mkopo kutoka FC Porto ya Ureno, alipomruka beki mmoja ndani ya eneo la hatari kabla ya kupiga shuti kali lililojaa kambani.

Mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Uturuki Kenan Yildiz alifunga la tatu baada ya dakika 31, akittumia vizuri nafasi nje kidogo ya box na kukevu mpira uliopita karibu na mlingoti wa goli (near post).

Kolo Muani alifunga bao lake la pili kwa kumalizia kwa ustadi mpira wa Khéphren Thuram-Ulien mnamo dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza. Bao la beki wa kati wa Al Ain Kouame Autonne la offside lilikataliwa kabla ya Conceicao kufunga tena, akinufaika na mpira mwingine wa ‘deflection’.

Huenda Kolo Muani angekamilisha hat-trick lakini kipa Rui Patricio akazima shambulio hilo kabla ya Douglas Luiz kupiga shuti kali lililopita seentimita chavhe nje ya goli. Juventus, ambao walimaliza katika nafasi ya nne kwenye Serie A, wanatumai kufidia msimu usio na taji wala mafanikio nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button