Kwingineko

Jina la Ten Hag latua Ajax

AMSTERDAM:MKURUGENZI wa mashindano wa klabu ya ligi kuu ya Uholanzi Ajax Amsterdam, Alex Kroes amesema kuna uwezekano mkubwa wa meneja wao zamani United Erik ten Hag kurejea kukinoa kikosi hicho kuelekea msimu mpya baada ya kocha waliyekua naye msimu huu unamalizika Francesco Farioli kubwaga manyanga.

Alex Kroes amekiambia kituo cha televisheni cha NOS cha nchini Nederlands kuwa tayari wana mazungumzo na Ten Hag ambaye hana kazi tangu alipofurushwa na Manchester United mwezi Oktoba mwaka jana ili kuichukua mikoba ya Farioli aliyeacha kazi jana jumatatu

“Erik ten Hag amekuwa kwenye orodha ya makocha tunaowatamani kwa muda mrefu, anajulikana na alifanya kazi nzuri sana alipokuwa hapa. Nilizungumza nae kwa kifupi Jumapili alipokuja uwanjani kushuhudia mchezo wetu dhidi ya FC Twente” – Amesema Kroes

Ikiwa atatua Ajax haitakuwa mara ya kwanza kwa Ten Hag mwenye umri wa miaka 55, amewahi kukinoa kikosi hicho kuanzia mwaka 2018 mpaka 2022, akishinda makombe matatu na kuipeleka klabu hiyo kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya wakiwa wameanzia katika hatua za awali kabisa.

Farioli alitangaza kujiuzulu jana Jumatatu lakini tayari alishaamua kuondoka baada ya ‘sare ya ajabu’ kwenye mchezo wao dhidi ya Groningen waliokuwa pungufu Jumatano iliyopita wakati Ajax iliporuhusu uongozi wao wa 2-1 kupinduliwa dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika na kuiaga nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Eredivisie kwa PSV.

Related Articles

Back to top button