Kwingineko

Jezi za Barca, PSG kupigwa mnada

BARCELONA: KLABU za Barcelona na Paris Saint-Germain (PSG) watazipiga mnada jezi zilizovaliwa na wachezaji wao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ulaya wa Jana Jumatano ili kuisaidia taasisi ya binti wa kocha Luis Enrique ambaye kwa sasa ni marehemu.

Xana Enrique, binti wa kocha wa PSG, alifariki dunia mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 9 kufuatia kuugua moja ya aina tata ya saratani ya mfupa.

Wachezaji wa PSG walivaa nembo ya Xana Foundation kwenye jezi zao, ambazo zitapigwa mnada na mapato yote kwenda kwenye kwenye akaunti maalum za taasisi ya Xana Foundation.

Kwa upande wake FC Barcelona ilisema mapato ya mnada wa jezi zake yataenda kwenye programu ya Blaugrana Wristbands, ambayo itatoa mchango huo Kwenda kwenye taasisi ya Xana Foundation.

Taasisi hiyo inayoongozwa na kocha Luis Enrique inatoa msaada wa kimatibabu, kijamii na kihisia kwa watoto walio na magonjwa makubwa Pamoja na familia zao. Luis Enrique aliichezea Barcelona kabla ya kuwa kocha wa klabu hiyo ya Catalan.

Related Articles

Back to top button