Jennifer Lopez: Nipo vizuri kuliko nilivyokuwa na mpenzi

MADRID: MUIGIZAJI na mwanamuziki Jennifer Lopez anataka ulimwengu ujue kuwa anafanya vizuri zaidi kuliko hapo awali alipokuwa katika ndoa na Ben Affleck.
Jennifer na Ben Affleck waliachana miaka miwili baada ya kufunga ndoa na talaka yao ilikamilishwa Februari mwaka huu 2025.
Mwanamuziki huyo ameachia wimbo wake mpya ‘Wreckage of You’ ambapo katika mashairi ya wimbo huo yanaelezea kuhuwu namna anavyoendelea kuwa bora zaidia baada ya kutroka katika ndoa huku akiamini ataendelea kuwa hivyo hadi mwisho wake.
Wimbo huo ni sehemu ya onesho lake alilofanya nchini Uhispania, alioutambulisha kwa kusema: “Huu ni wimbo mpya ambao nataka kuuimba kwa mara ya kwanza usiku wa leo. Wimbo huu ulinijia nikiwa nimeamka usiku na nilaandika usikukucha.” Video ilisambaa alivyokuwa akieleza na shabiki wake mmoja baada ya kuiweka katika ukurasa wake wa instagram.
“Kwa sababu yako, mimi ni mwenye nguvu zaidi, mwenye busara zaidi. Bora zaidi kuliko nilivyowahi kuwa. Sitakuruhusu tena, tena, uniage tena. Ilikuwa kamili wakati ulinifanya niamini, kwa kweli ilikuwa kubwa zaidi kwangu, na ilinifanya kuwa na nguvu, nguvu, kuzuia risasi. Sasa niangalie nikipanda kutoka kwenye uharibifu wako.” Baadhi ya mistari katika wimbo huo.