
LAS VEGAS:MWANAMUZIKI na mcheza filamu Jennifer Lopez alishangaza mashabiki wake waliokuwepo jukwaani wakimshuhudia pamoja na wale waliokuwa wakimtazama kupitia runingani baada ya kuwabusu baadhi ya wanenguaji wake alipokuwa akifanya onesho la ufunguzi wa Tuzo za Muziki za Marekani za 2025 (AMAs) zilizofanyika huko Las Vegas Marekani.
Mabusu ya Jeniffer Lopez yalianza wakati alipokuwa akiimba wimbo wa ‘Lose Control ndipo akamfuata mnenguaji wake mmoja Teddy Swims na kumbusu kasha akawafuata na wengine na kuwabusu bila kujali jinsia zao.
JLo akiwabusu wacheza densi wake wa kiume na wa kike wakati wa onesho hilo jambo lililoibua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakimuhusisha na sonona kutokana na kitendo hicho kilitafsiriwa tofauti na mashabiki hao wakimuhusisha kuachwa kwake na aliyekuwa mume wake Ben Affleck kwa miezi kadhaa sasa.
Kabla ya kugawa mabusu kwa wanenguaji wake Jennifer akiimba toleo la polepole la wimbo wake wa mwaka 2012 wa ‘Dance Again’.
Nyota huyo wa muziki wa pop alitinga kwenye vibao bora mwaka huu, vikiwemo ‘Not Like Us’ wa Kendrick Lamar, ‘NUEVAYoL’ wa Bad Bunny na ‘Birds of a Feather’ wa Billie Eilish.
Pia aliigiza kwenye kipindi cha Doechii cha ‘Denial Is a River’, Wimbo wa ‘A Bar’ wa Shaboozey na Bruno Mars na APT ya Rosé.




