Mastaa

Iyabo Ojo:Sitaolewa na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Muziki

NIGERIA: MUIGIZAJI maarufu wa Nollywood Iyabo Ojo amefichua kwa nini hawezi kuolewa na mtendaji maarufu wa muziki wa Nigeria, Paulo.

Akizungumza wakati wa mahojiano na TVC, Iyabo Ojo alifichua kuwa malengo ya uhusiano wao si ya ndoa, na wanafurahi kwa namna wanavyoishi na kushirikiana.

Akiondoa mipango ya ndoa, Iyabo Ojo amesema, “Anathamini usiri wake na hatuna mpango wa ndoa.”

Akielezea mienendo ya uhusiano wao, amesema, “Kwa sababu ya asili ya kazi yangu, mimi ni mchapakazi sana na Paulo pia ni mtu wa kufanya kazi. Huyo mwanaume wa Igbo anapenda kufanya kazi. Kwangu, kuna wakati nataka kuwa peke yangu; ninapojisikia kuwa peke yangu, nafunga virago na kurudi nyumbani kwangu. Hatujawahi kupingana na hilo kwa sababu anaelewa na ndivyo tunavyoishi.”

“Hatutaki ndoa, tunaishi kwa furaha.”

DAILY POST imeeleza kuwa Iyabo Ojo alithibitisha uhusiano wake na Paulo mnamo Desemba 2022, wakati wa siku yake ya kuzaliwa alipokuwa anatimiza miaka 45.

Related Articles

Back to top button