Tetesi

Inter kutoa Euro 45 milioni kwa Lookman

ITALIA: TIMU ya soka ya Inter Milan ya Italia imepanga kuongeza ofa kwa fowadi wa Atalanta, Ademola Lookman hadi euro milioni 45 wiki ili kumnasa mchezaji huyo bora mwenye tuzo ya Afrika.

Kwa mujibu wa PUNCH timu hiyo imeendelea kumsaka mchezaji huyo kutoka Nigeria bila kukata tamaa.

Mhariri wa Corriere dello Sport Ivan Zazzaroni alifichua kwamba Nerazzurri wana bajeti ya majira ya joto ya Euro milioni 100 kutoka kwa wamiliki wa Oaktree Capital na watatanguliza usajili wa Lookman kama shabaha yao kuu ili kuimarisha sehemu ya ushambuliaji katika timu yao.

“Oaktree wameweka euro100 milioni kwa ajili ya uhamisho,” Zazzaroni aliandika katika chapisho la Instagram. “Lookman ndio lengo lao la kwanza.”

Mhariri huyo alitabiri kwamba wiki ijayo Inter itaongeza ofa ya hadi Euro milioni 45 kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo.

Ombi la awali la Inter la euro milioni 40 lilikataliwa na Atalanta, ambao wanaripotiwa kutaka euro milioni 50 kwa ajili ya winga huyo mwenye umri wa miaka 27.

Licha ya mvutano unaoendelea kati ya vilabu hivyo, Lookman tayari amekubali makubaliano ya kibinafsi na Inter kwa mkataba wa miaka mingi wenye thamani ya karibu euro milioni 4 kwa msimu huku akiweka mipango yake mipya kwa klabu hiyo ya San Siro.

Mchezaji huyo wa zamani wa RB Leipzig na Leicester City amekataa nia ya Barcelona, Atlético Madrid na Napoli ili kujiunga na Nerazzurri.

Napoli, chini ya kocha mpya Antonio Conte, walikuwa na matumaini ya kumtumia Giacomo Raspadori katika makubaliano ya kubadilishana na Lookman, lakini Mnigeria huyo alikataa ofa hiyo, huku maslahi ya Barcelona yakikwamishwa na matatizo yao ya kifedha yaliyokuwa yakiendelea.

Nia ya Inter ya kuongeza ofa yao inakuja wakati Lookman anakaribia kupona kabisa kutokana na jeraha na inawakilisha mabadiliko makubwa kutoka kwa msimamo wao wa awali wa kukataa ofa chini ya euro milioni 40

Related Articles

Back to top button