Ligi Kuu

Ibenge ainua mapanga Dar Dabi

DODOMA: KOCHA Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge amesema hawana sababu ya kuficha mbinu zao kuelekea mchezo ujao dhidi ya Yanga akisisitiza kuwa wapinzani wao tayari wanaifahamu vizuri timu yake kutokana na mechi nyingi walizocheza msimu huu.

Ibenge amesema ni jambo la kawaida kwa timu pinzani kufuatilia michezo ya wapinzani wao ili kujua mbinu na mfumo wanaotumia kabla ya kukutana uwanjani.

“Ni jambo la kawaida. Kama ningekuwa katika hali hiyo pia ningekuja kuutazama mchezo wa mpinzani wangu,” amesema Ibenge baada ya kuuliza swali ya waandishi wa habari kuhusu uwepo WA wapinzani wao wajao kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Dodoma Jiji.

Amesema kuwa Azam FC haina kitu cha kuficha kwa kuwa tayari imecheza mechi kadhaa ambazo zinaonesha wazi mfumo wao wa uchezaji.

“Hatuwezi kuficha chochote. Tayari tumeshacheza karibu mechi 10, hivyo kama mtu anataka kuona namna tunavyocheza anaweza kuangalia mechi hizo.”

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Ibenge amesema timu yake itaendelea kujipanga vizuri ili kupata matokeo mazuri katika mchezo huo muhimu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button