Kwingineko

Hisia kali Estevao akiaga Palmeiras

PHILADELPHIA, Mchezaji chipukizi wa Palmeiras Estevao Willian alijawa na hisia kali waakati akiwaaga mashabiki na wachezaji wa klabu hiyo baada ya kupoteza mabao 2-1 mbele ya Chelsea katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia la Klabu alfajiri ya leo.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye anajiunga na Chelsea baada ya michuano hiyo, alifunga bao zuri la kusawazisha lakini halikumpunguzia maumivu moyoni kwani bao la kujifunga la golikipa wao liliipeleka timu hiyo ya Ligi Kuu ya England nusu fainali.

Goli la Estevao la dakika ya 53 lilionesha uwezo mkubwa ambao umemfanya kuwa mmoja wa mawinga wa kibrazil wanaotarajiwa kung’aa zaidi na kuacha maswali magumu juu ya namna ya kuziba pengo ambalo ataacha katika timu yake ya Palmeiras kwani ndiye mchezaji bora hata wa mechi hiyo.

“Nimefurahi kuisaidia timu yangu kupata bao. Kwa bahati mbaya, hayakuwa matokeo tuliyotaka, lakini nadhani ni sawa. Tulijitolea kwa nguvu zetu zote uwanjani, na hilo ndilo jambo muhimu.” amesema Estevao

Kinda huyo hakusita kumwaga sifa kwa kocha wa Palmeiras Abel Ferreira, ambaye alimwita “baba” na akasifu jitihada za kocha huyo katika kumsaidia kukua kama mchezaji.

“Kocha, asante sana kwa kila kitu, Alinifundisha kucheza kwa mbinu, na hilo limekuwa jambo muhimu sana kwangu. Palmeiras ilinifungulia milango, na nilifurahi sana hapa siku zote nitaibeba klabu hii moyoni mwangu”.

Related Articles

Back to top button