Kwingineko

Henderson aondoka Ajax

AMSTERDAM: Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya England Jordan Henderson anaondoka kwa wababe wa soka Uholanzi Ajax mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kutamatika kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Ajax yenye makao yake makuu jijini Amsterdam katika kipindi ambacho vigogo hao wakiwa moto mwezi Januari mwaka 2024, miezi sita pekee baada ya uhamisho wake kutoka Liverpool kwenda Saudi Arabia kuzua utata kuhusu msimamo wake juu ya mapenzi ya jinsi moja.

Henderson alimaliza haraka utata huo alipohamia Ajax huku klabu hiyo ikimteua kuwa nahodha wa klabu na akacheza mechi 57 akiwa na jezi ya Ajax iliyopewa umaarufu mkubwa na wachezaji nguli kama Johan Cruyff na Dennis Bergkamp.

Henderson aliisaidia Ajax kuzinduka kutoka katika moja ya misimu yao mibaya na kushindania taji la Eredivisie mwaka jana. Lakini walipoteza fursa ya kutwaa ubingwa huo wakipoteza uongozi wa pointi tisa wakiwa na mechi tano pekee za kucheza na kuwapa taji wapinzani wao wakubwa PSV Eindhoven.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Ajax Alex Kroes alimuelezea Henderson kama nahodha wa kweli ndani na nje ya uwanja. Kroes amesema kupitia mawazo yake na sifa za uongozi Henderson alikuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia timu hiyo kufuzu UEFA Champions League.

Kiwango cha Henderson akiwa Ajax kilimfanya arudishwe haraka kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya England chini ya Thomas Tuchel mwezi Machi mwaka huu huku akishukuru kwa fursa ya kuonekana ndani ya klabu hiyo ya Amsterdam.

Related Articles

Back to top button