EPLKwingineko

Haaland: Sikutarajia kuwa na kiwango bora

MSHAMBULIAJI wa Manchester City Erling, Erling Haaland amekiri kuvunja kwake rekodi katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu England(EPL) kumepitiliza matarajio yake.

Amesema hayo jijini London, England baada ya kupokea tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya Chama cha Waandishi wa Habari za Soka(FWA).

“Nilitarajia kufanya vizuri lakini, hivi nilivyofanya, sikutarajia. Nitafanya kila niwezalo kufikia mambo mazuri kwenye fainali zinazotukabili na natumaini tutashinda zote mbili,”amesema Haaland.

Haaland mwenye umri wa miaka 22 amepata asilimia 92 ya kura kushinda tuzo hiyo akiwapiku Bukayo Saka na Martin Odegaard wa Arsenal.

Amefunga mabao 52 katika michezo 51 ya City katika EPL kabla ya mchezo wa mwisho ugenini dhidi ya Brentford Mei 28.

Alijiunga na Man City msimu unaokwisha akitokea Borussia Dortmund kwa uhamisho wa pauni milioni 51 sawa na shilingi bilioni 146.6.

City itaikabili Inter Milan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Juni 10 jijini Istanbul, wiki moja baada ya kucheza mechi ya fainali Kombe la FA dhidi ya Manchester United ikiwa tayari ni bingwa wa EPL.

Related Articles

Back to top button