EPL

Haaland ajifunga miaka 9 Man City

MANCHESTER:ERLING Haaland, mshambuliaji nyota wa Manchester City, amesaini mkataba mpya wa kihistoria wa miaka 9 na nusu ambao utamuweka klabuni hapo hadi Juni 2034.
Mkataba huu unavunja rekodi ya mishahara ndani ya klabu, huku kipengele cha kuondoka kwa ada kubwa kikitarajiwa kuanza kutumika mwaka 2029.
Haaland, mwenye umri wa miaka 24, atakuwa na miaka 34 mkataba huo utakapomalizika na tangu alipojiunga na Manchester City mwaka 2022 akitokea Borussia Dortmund, Haaland amefunga mabao 111 katika mechi 126
Alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya City katika msimu wa kihistoria wa ‘Treble’ mwaka 2022/23 na pia alishinda mataji ya FA Cup, UEFA Super Cup, na Community Shield msimu uliopita.
Awali, mshahara wake ulikuwa £375,000 kwa wiki, lakini sasa mkataba huu mpya, wenye bonasi kubwa , unamfanya apokee zaidi ya £850,000 kwa wiki (pamoja na bonasi).
Akizungumzia mkataba huo, Haaland alisema, “Nimefurahi sana na najivunia. Uamuzi huu ulikuwa rahisi kutokana na msaada mkubwa kutoka kwa bodi, viongozi, na Pep Guardiola.”
Mashabiki wa City mnafurahi mkiwa wapi kusikia taarifa hii?

Related Articles

Back to top button